Mwanamke afariki kanisani alikopelekwa kuombewa

0
40

Polisi nchini Uganda wanachunguza kifo cha mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rosette Najjuma (59) kilichotokea Jumatano, Februari 8 wakati wa ibada katika Kanisa la Christian Life eneo la Kigundu, jijini Kampala.

Msemaji Msaidizi wa polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigyire amesema mwanamke huyo alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Mulago kwa muda wa miaka mitatu iliyopita licha ya kuwa hakuna ugonjwa wowote uliogunduliwa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa rafiki zake waliamua kumtafutia msaada wa kiimani na ndipo walimpeleka kwenye kanisa la Mchungaji Jackson Ssenyonga ili kuombewa na ndipo alizirai na kufariki wakati ibada ikiendelea.

“Licha ya kufanyiwa vipimo mbalimbali, hakuna ugonjwa uliogundulika na ndipo aliletwa kanisani. Inaripotiwa kwamba aliaga dunia takribani saa kumi jioni wakati wa ibada ya maombi,” amesema Owoyesigyire.

Send this to a friend