Mwanamke afukuzwa na wanakijiji kwa tuhuma za uchawi

0
56

Mwanamke mwenye umri wa takribani miaka 60, mkazi wa Kitongoji cha Ipapa kilichopo Kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, amefukuzwa kutoka kijijini hapo na wananchi baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo limejiri baada ya wananchi hao kudai kumkuta mwanamke huyo akiwa hajavaa nguo kwenye nyumba ya jirani yake majira ya saa 8 usiku, hali iliyozua hisia miongoni mwa wanakijiji kwamba alikuwa akijihusisha na imani za kishirikina.

Wananchi hao wamedai mwanamke huyo amekuwa akishutumiwa kwa imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha madhara kwa majirani zake ikiwa ni pamoja na kuharibu mazao na mifugo yao.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kitongoji hicho, Nelbati Kasekwa, amewapongeza wananchi hao kwa kutojichukulia sheria mkononi na kueleza kuwa mtuhumiwa yuko salama chini ya jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Send this to a friend