Mwanamke ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto

0
18

• Shani Suleiman (35) amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 12.
• Mwanamke huyo alianza mchezo huo tangu mtoto huyo akiwa darasa la tatu.

Mahakama ya Rufani Tanzania imemuhukumu kifungo cha maisha jela mwanamke mmoja mkazi wa Morogoro, Shani Suleiman (35) kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12.

Inadaiwa mwanamke huyo alikamatwa Januari 13, 2019 baada ya mama mzazi wa mtoto huyo pamoja na rafiki yake kuandaa mtego katika nyumba ya mwanamke huyo ambapo walirekodi tukio hilo kwa kutumia simu janja.

Uwekaji kope, lenzi machoni chanzo cha upofu

Hii ni baada ya mtoto kumweleza mama yake kuwa mama Shani maarufu kama mama Shafii amekuwa akimwambia amwingilie mara kwa mara na wakati mwingine kinyume cha maumbile kwa kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2019.

Kwa mujibu wa ushahidi alioutoa mtoto huyo mahakamani hapo, alidai mwanamke huyo alianza kufanya mchezo huo tangu mwaka 2016 alipokuwa darasa la tatu ambapo alimshawishi aingie chumbani kwake na siku nyingine alimpeleka katika nyumba ambayo ilikuwa haijamalizika kisha kufanya kitendo hicho.

Send this to a friend