Mwanamke akamatwa akijaribu kupenyeza bangi kwa mumewe aliyeko gerezani

0
37

Mwanamke mmoja nchini Kenya, Caroline Imenza amekamatwa siku ya Jumapili kwa kujaribu kupenyeza bangi kwa mumewe ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa polisi katika Kituo cha Polisi cha Gilgil.

Mwanamke huyo aliingia katika kituo hicho cha polisi saa 12 asubuhi akiwa na chupa ya chai na mkate na kuomba kuonana na mumewe Stephen Nyabuto ambaye alikuwa amekamatwa.

Imenza mwenye umri wa miaka 30 alikuwa ameingiza vipande vya bangi kwenye mkate huo akitarajia kuvikabidhi kwa mumewe bila ya kugundulika kwa maafisa wa polisi.

Hata hivyo, afisa wa polisi aliyekuwa zamu aligundua mpango huo na kuendelea kuufungua mkate huo, ambapo aligundua roli 5 za bangi, sigara 5 na sanduku la kiberiti.

“Alifunua mkate huo na kukuta korongo lenye mwinuko ambapo ni kawaida kwa mikate ya siku hizi, lakini alipoendelea kuukagua alikutana na roli 5 za bangi, sigara tano na sanduku la kiberiti,” imeeleza ripoti.

Majambazi wasimamisha mahubiri kanisani na kuwaibia waumini

Afisa huyo alimzuia Imenza na kumpeleka kwenye chumba kilichotengwa kwa ajili ya kesi zinazohusiana na jinsia, ambapo alimfanyia uchunguzi wa kina mshukiwa na kumkuta na roli 80 za bangi kutoka kwenye nguo za ndani za Imenza.

Mtuhumiwa alifanya jitihada za kuwahonga maofisa hao Sh. 2,000 [sawa na TZS 38,137] ili kupata uhuru wake lakini hakuweza kufanikiwa.

Send this to a friend