Mwanamke akamatwa kwa kupeleka maiti benki ili asaini mkopo

0
44

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Érika de Souza Vieira Nunes wa nchini Brazil amekamatwa baada ya kupeleka maiti benki, akitumaini kwamba ingemsaidia kupata mkopo.

Nunes amenaswa kwenye video na wafanyakazi wa benki akiupeleka mwili wa Paulo Roberta Braga (68) kwenye tawi la benki ya Rio De Janeiro akiwa kwenye kiti cha magurudumu huku akisikika akimwita Braga ‘mjomba’ na kujaribu kumtaka atie saini karatasi iliyokuwa mbele yake.

“Mjomba, unasikiliza?” Unahitaji kusaini. Usipotia saini hakuna njia, kwa sababu siwezi kusaini badala yako,” Nunes anasikika akisema kabla ya kuchukua kalamu na kuilazimisha mikononi mwa marehemu.

“Saini ili usinitie maumivu ya kichwa tena, siwezi kuvumilia tena,” aliuambia mwili.

Baada ya wafanyakazi kuingiwa na wasiwasi juu ya afya ya Braga waliwaita polisi ambao waligundua kuwa Nunes ameleta mwili wa mtu aliyefariki takribani saa mbili zilizopita, na kisha kufunguliwa kesi ya kujaribu kuiba.

Hata hivyo, mwanasheria wa Nunes ameeleza kwamba Braga alikuwa hai wakati akiingizwa benki, nakwamba Nunes hana hatia.

Send this to a friend