Mwanamke aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kutoitunza vizuri mimba yake aachiwa huru

0
38

Mwanamke nchini El Salvador aliyetambulika kwa jina la Lilian (28) ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kutumikia adhabu kwa miaka nane kutokana na kifo cha mtoto wake aliyezaliwa hospitalini.

Lilian alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela mwaka 2015 baada ya kukutwa na hatia kufanya uzembe na kusababisha kifo cha mtoto wake japokuwa amekuwa akipinga tuhuma hizo na kudai hakuwahi kukusudia kufanya hivyo.

Mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike mwaka 2015, lakini mtoto huyo alipata matatizo ya kiafya na kufariki hospitalini siku tatu baadaye hivyo waendesha mashtaka walimshtaki kwa kutomtunza wakati wa ujauzito wake, na kufanya uzembe uliosababisha kifo.

Mwaka wa 2023, mahakama ilipitia upya hukumu yake na kuamuru aachiliwe.

Mwalimu bora wa kike ashitakiwa kwa ubakaji wa wanafunzi

Kulingana na taarifa, Lilian alikuwa mwanamke wa mwisho kati ya wanawake 73 waliokuwa wamefungwa baada ya kuhukumiwa kwa uzembe uliosababisha vifo, kutoa mimba au dharura nyingine za uzazi.

Nchini El Salvador imewekwa sheria kali juu ya utoaji mimba na makumi ya wanawake wanaaminika kufungwa kimakosa nchini humo kwa tuhuma za kutoa mimba.

Wale wanaopatikana na hatia ya kutoa ujauzito wao wanakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka miwili hadi minane gerezani lakini mara nyingi shtaka hubadilishwa na kuwa mauaji ya kuchochewa na adhabu yake ni kifungo cha chini cha miaka 30.

Send this to a friend