Mwanamke aliyeripotiwa kufariki miaka mitano arejea na kusimulia kisa kizima

0
36

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Mwashi Lutema (33) anayedaiwa kufariki takribani miaka mitano iliyopita ameonekana akiwa hai katika Kijiji cha Kamalampaka Wilaya ya Mlele mkoani Katavi na kuzua taharuki ikiwemo ndugu na majirani wa eneo hilo.

Wakitoa ushuhuda wa tukio hilo, ndugu wa mwanamke huyo wamesema ndugu yao alifariki dunia Aprili 2018 kwa maradhi ya kifua baada ya kupelekwa kwa mganga kwa ajili ya matibabu bila mafanikio na kufanyiwa taratibu zote za mazishi.

“Tukio la kuonekana akiwa hai nilisikia baada ya kupigiwa simu na kwenda kushuhudia na kweli nikakuta ni mwenyewe, mwanzo sikuamini ila nilipomuona kwa sura na kuongea naye ndipo nilipoamini. Alikuwa kwenye ofisi za Mtendaji waliniambia ametokea Mpanda maeneo yasiyojulikana,” ameeleza shemeji yake, Elias Maduhu.

Mchungaji ahukumiwa miaka 70 kwa kubaka watoto

Akisimulia kisa hicho mwanamke huyo anayedaiwa kufariki amesema kuna watu ambao baadhi anawakumbuka na wengine hawafahamu wakiwemo wanawake, wanaume, vijana wa kike na wakiume pamoja na wazee, walimchukua na kumpeleka sehemu isiyojulikana na kumtesa lakini mwisho alifanikiwa kuwatoroka.

“Huko nillikuwa naishi mazingira magumu, nilikuwa nakula vitu ambavyo havieleweki kama mchanga, sabuni na matope, mara wanibake wamenitesa sana, wamaenipiga wakaniumiza ila hawajanifanyisha kazi yoyote ngumu zaidi ya kunitesa, amesimulia.

Akithibitisha tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kamsisi, Leonard Kiyungi amesema mwanamke huyo anatokea katika eneo hilo na wameshtushwa na tukio hilo ambalo halijawahi kutokea katika Wilaya hiyo.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend