Mwanamke ashtakiwa kwa kuiba majeneza mawili

0
44

Mwanamke mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kwa tuhuma za kuiba majeneza mawili na vishikio 26 vya majeneza kutoka kwenye kituo cha uuzaji majeneza cha Mtakatifu Augustine ambacho alikabidhiwa kama msimamizi.

Maureen Khikani (30-40) amefikishwa mbele ya mahakama ya Nairobi siku ya Ijumaa kujibu mashtaka hayo, ambapo kwa upande wa mashtaka unadai Maureen aliiba majeneza yenye thamani ya TZS milioni 1.5 na vishikizo vyenye thamani ya TZS milioni 2.02.

Kwa upande wa mshitakiwa, amekanusha mashtaka yote dhidi yake huku Wakili wake akiiomba mahakama kumuachiliwa mteja wake kwa masharti nafuu zaidi na kusisitiza kuwa mshitakiwa ni mama siye na mume.

Watanzania 28 wahukumiwa kwa kuingia Afrika Kusini kinyume cha sheria

Hakimu wa Mahakama ya Milimani, Ben Mark Ekhubi amemuachilia kwa dhamana ya TZS milioni 3.4.

Send this to a friend