
Polisi nchini Korea Kusini wamesema wanatafuta kibali cha kumkamata mwanamke (20) aliyesababisha moto katika jengo la makazi wakati akijaribu kuua mende kwa kutumia kiberiti na dawa ya kupuliza yenye kemikali.
Tukio hilo la moto limepelekea jirani mmoja mwanamke kupoteza maisha baada ya kuanguka kutoka ghorofani wakati akijaribu kutoka ndani ya jengo kupitia dirishani.
Polisi katika jiji la kaskazini la Osan wamesema mwanamke huyo anaweza kufunguliwa mashtaka ya kusababisha moto kwa bahati mbaya na kusababisha kifo kwa uzembe.







