Mwanamuziki AKA wa Afrika Kusini auawa kwa kupigwa risasi

0
37

Jeshi la Polisi jijini Durban nchini Afrika Kusini limethibitisha kuwa rapa Kiernan Forbes, maarufu AKA, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi akiwa amesimama pembezoni mwa barabara.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtu mwingine anayeaminika kuwa mlinzi wa AKA amejeruhiwa huku mtu mwingine ambaye hajatambulisha lakini ikiaminika alikuwa mtu wa karibu na rapa huyo amefariki pia.

AKA alikuwa amesimama nje ya mgahawa kabla ya kumiminiwa risasi kutoka kwenye gari lililokuwa katika Barabara ya Florida ambapo taarifa ambazo sio rasmi zinaeleza kuwa risasi hizo zilitoka kwenye magari mawili.

Rafiki yake, Da Les, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika akionesha kushtushwa na kifo hicho;

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mitandao ya kijamii AKA alikuwa anatarajia kutumbuiza katika klabu ya usiku ya YUGO jijini Durban, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi yake ya kuzaliwa.

AKA ni mmoja wa wasanii wa Afrika Kusini wanaofahamika zaidi nchini Tanzania kutokana na kufanya kazi na wasanii wa Tanzania akiwemo Joh Makini katika wimbo wa ‘Don’t Bother’ na Diamond Platnumz katika wimbo ‘Make Me Sing.’

 

 

Send this to a friend