Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia askari wanne wa maliasili kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Semeni Hamisi (34), mkazi wa Kijiji cha Nyamigota, Kata ya Nyamigota, baada ya kukutwa ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Samina akiokota kuni za matumizi ya nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe amesema miongoni mwa watu wanaoshikiliwa yupo pia mwananchi mwingine aliyekuwa miongoni mwa watu walioingia kwenye hifadhi ambaye baada ya mahojiano hatua za kisheria zitafuata dhidi yake.
Lushoto: Wazee wakausha maji baada ya mradi kuanzishwa bila kupewa taarifa
“Nachotaka niseme ndugu zangu wananchi, ni lazima ufike mahala ujue ni mahala gani umekatazwa kufanya jambo lolote la namna gani katika eneo hilo, lakini la pili ukimkuta mtu ana silaha ya aina yoyote, hata kama ni panga, rungu au bunduki usifanye chochote kwa sababu huwezi kujua akili yake itamtuma nini,” ameeleza.