Mwanasiasa afungwa kwa njama za kuiba figo

0
39

Mahakama ya London imemfunga jela miaka tisa na miezi nane mwanasiasa wa Nigeria, Ike Ekweremadu (60) baada ya kufanya njama ya kumpandikiza figo binti yake kutoka kwa kijana waliyemsafirisha kutoka Lagos.

Mahakama imemhukumu pia mke wake, Beatrice (56) kifungo cha miaka minne na miezi sita pamoja na daktari anayeishi London, Obinna Obeta (51) kifungo cha miaka kumi kwa kushirikiana kutekeleza mpango huo.

Wote watatu wamepatikana na hatia kwa kumsafirisha mfanyabiashara wa mtaani mwenye umri wa miaka 21 hadi Uingereza katika kitengo binafsi cha wagonjwa wa figo hospitali ya Royal Free nchini humo, ili kumtoa figo yake kinyume cha sheria kwa ajili ya upandikizaji wa binti yao Sonia ambaye ni mgonjwa.

China yapunguza mikopo kwa Kenya 

Waendesha mashtaka wamesema Ekweremadu na mkewe walimleta kijana huyo London mwezi Februari mwaka jana wakimuahidi kitita cha pesa kwa ajili ya kiungo chake na ahadi ya kufanya kazi nchini Uingereza.

Mapema wiki hii Rais wa bunge la seneti la Nigeria, Ahmad Lawan aliiandikia mamlaka ya mahakama ya Uingereza akitaka imhurumie Ekweremadu kwa niaba ya seneti kwa kuwa lilikuwa kosa lake la kwanza.

Send this to a friend