Mwanaume adaiwa kuwaua wanae watatu kisa wanapiga kelele

0
12

Maafisa wa Polisi nchini Thailand wanamshikilia mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Songsak Songsaeng kwa tuhuma za kuwapiga hadi kuwaua watoto wake watatu.

Songsak anashtakiwa kwa kumuua binti yake wa miaka miwili, pia anadaiwa kufanya tukio hilo kwa watoto wake wengine wachanga wawili wa kiume katika ndoa yake ya awali.

Polisi wanasema mwanaume huyo anadai kuwa na historia ya ugonjwa wa akili na kwamba aliwaua watoto wake kwa sababu hakuweza kuvumilia sauti ya kilio chao.

Mke wake wa sasa ameshikiliwa kwa kifo cha binti yao wa miaka miwili na mke wa zamani pia ameshikiliwa kwa kifo cha watoto wao wa kiume wa wili ambao mwanaume huyo anashtakiwa kwa vifo vyao.

Mmoja wa binti zake mwenye umri wa miaka 12 aliwaambia polisi kwamba wazazi wao walimpiga dada yake na kusababisha kifo chake.

Send this to a friend