Mwanaume aiba ng’ombe na kuiuza ili amnunuliwe mchumba wake zawadi

0
57

Mwanamume mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Andati amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Kakamega nchini Kenya baada ya kukiri kuiba ng’ombe kwa nia ya kumshawishi mpenzi wake kuolewa naye.

Andati ameileza mahakama kwamba aliuza ng’ombe huyo kwa Ksh20,000 [sawa na TZS laki 382.7] ili amnunulie mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali anayetoka kijiji cha Isulu, Ikolomani Kaunti ya Kakamega.

Miaka 30 jela kwa kumbaka mlemavu wa viungo na akili

Aidha, mahakama imeeleza kuwa mshukiwa huyo alivamia nyumba ya Jane Shimenga Jumatano usiku katika kijiji jirani cha Burendwa kisha kuondoka na ng’ombe huyo.

Hata hivyo, mahakama imemtaka Andati kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega kwa ajili ya kutathminiwa afya yake ya kiakili, kisha atafikishwa tena mahakamani hapo Alhamisi ya wiki ijayo.

Send this to a friend