Mwanaume aishi siku 100 akiwa na moyo bandia

0
1

Mwanaume mmoja wa Australia ameishi kwa siku 100 na moyo bandia wa titani wakati akisubiri upandikizaji wa moyo kutoka kwa mfadhili, na kuweka rekodi ya kuishi siku nyingi kwa teknolojia hiyo.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, alikua mtu wa kwanza duniani kuruhusiwa kutoka hospitalini akiwa na kifaa hicho, ambacho kilimwezesha kuendelea kuishi hadi alipopata moyo wa mfadhili mapema mwezi huu.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano na Hospitali ya St Vincent, Chuo Kikuu cha Monash na kampuni ya BiVACOR (kampuni ya Marekani na Australia iliyoanzisha kifaa hicho), mwanaume huyo aliyekuwa na ugonjwa mbaya wa moyo kwa sasa anaendelea vizuri.

Uwezo wa kifaa hicho kumuwezesha kuishi kwa muda mrefu unasherehekewa kama ishara kwamba moyo bandia unaweza kuwa suluhisho la muda mrefu kwa watu wanaougua matatizo ya moyo. Hata hivyo, kifaa hicho bado kinajaribiwa na hakijaidhinishwa kwa matumizi ya jumla.