Mwanaume ajichoma moto baada ya mkewe kukataa kumpikia kuku

0
51

Polisi nchini Kenya wanachunguza tukio la mwanamume mmoja aliyefariki kwa kujichoma moto baada ya mkewe kudaiwa kukataa kupika kuku nyumbani kwao Uriri, Kaunti ya Migori.

Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la John Rugala (45) alijifungia ndani ya nyumba yao kisha kujichoma moto baada ya mke wake kumtaka amwombe ruhusa binti yao ambaye alikuwa mmiliki wa kuku huyo.

Tarime: Auawa kwa kisu akigombania mwanamke baa

Inadaiwa marehemu alimtimua nyumbani mkewe kabla ya kuchukua uamuzi huo, huku juhudi za wananchi za kuuzima moto huo baada ya kufika eneo la tukio zikiambulia patupu.

Akizungumza Msaidizi wa Polisi, John Atonya amesema mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Migori Level Four kusubiri uchunguzi na kutoa wito kwa wanandoa kutafuta njia mbadala za kutatua migogoro yao.

Send this to a friend