Mwanaume akamatwa kwa kutangaza kujiuza

0
40

Polisi wa Kiisalmu (Hisbah) katika Jimbo la Kano nchini Nigeria wamemkamata Aliyu Na Idris (26) aliyezua gumzo mitandaoni siku chache zilizopita kwa kutangaza kuwa anajiuza kutokana na tatizo la umaskini.

Kamanda wa Hisbah amethibitisha kukamatwa  kwa kijana huyo na kuogeza kuwa kitendo chake cha  kutaka kujiuza kimezuiliwa kwenye sheria za Uislam, kwani haijalishi hali ya maisha yake,  huwezi kutaka kujiuza.

Akizungumza na chombo cha habari nchini humo alisema alikuwa na tatizo kubwa la kifedha na hivyo kuamua kujiuza kwa TZS milioni 113, kwa kusimama na bango barabarani likiwa na ujumbe kwamba atakuwa mtiifu kwa atakayemnunua.

“Uamuzi wa kujiuza umetokana na umaskini, nilipanga kuwapa wazazi wangu TZS milioni 55 mara tu nitakapopata mmunuzi, nilipe kodi TZS milioni 28, nimpe TZS milioni 12 kwa yeyote atakayenisaidia kupata mnunuzi, na zitakaazobaki ni za matumizi yangu,” alisema kabla ya kukamatwa.

Send this to a friend