Mwanaume mmoja nchini Kenya Joseph Odongo (81) ambaye alidhaniwa amefariki miaka 50 iliyopita amerejea nyumbani kwao baada ya kuiacha familia yake katika kijiji cha Riwa eneo la Homa Bay mwaka 1972.
Odongo ambaye aliondoka nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 30 na kwenda kuishi katika Mji wa Pwani Mombasa, amesema sababu ya yeye kukaa mbali na familia yake kwa miaka 51 ni kutaka kuepusha mzozo kati yake na mmoja wa ndugu zake ambaye kwa sasa ameaga dunia.
“Kule nilikuwa nasimamia nyumba, na nilihisi faraja nilipokuwa Mombasa, jambo ambalo lilikuwa tofauti nilipokuwa katika mji wangu wa Homa Bay,” anasema Odongo.
Mwanaume huyo aliiaga familia yake kuwa anakwenda katika fukwe za Sikri ambayo iko kilomita chache kutoka nyumbani kwao, na wana familia walidhani angerudi baada ya siku chache, lakini wiki ziligeuka kuwa miezi, na miezi ikageuka kuwa miaka, tangu wakati huo ikawa vigumu kuwasiliana naye na kujua aliko, ndipo familia yake ikatangaza kuwa amefariki.
Zipi sababu za mahakama kutamka kuwa ndoa iliyofungwa ni batili?
Mara baada ya kurudi nyumbani kwao, amekuta mali yake ambayo ni moja ya ardhi aliyorithi kutoka kwa wazazi wake iliyochukuliwa na watu wa familia yake ambao wameshafariki.
Wakati huo wote, Odongo hakuwa ameoa ingawa aliwahi kuwa na ndoto ya kuoa. Mmoja wa wazee wa kijiji hicho amesema “familia yake imuozeshe ili asiwe mtu wa kukaa peke yake, na apate msaada unaohitajika.”
Chanzo: BBC Swahili