Mwanaume aliyepotea kwa miaka 34 apatikana akiwa na familia mpya

0
33

Mwanaume mmoja kutoka Kisii nchini Kenya, Joseph Nyaanga aliyepotea miaka 34 iliyopita, amegunduliwa hivi karibuni akiishi na familia mpya katika mji wa Kabartonjo, Kaunti ya Baringo.

Mwanaume huyo ambaye familia yake ilidhani alikuwa amefariki, alitoweka kwa njia ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka 35, ambapo familia yake ilikata tamaa baada ya juhudi za kumtafuta katika vyumba vya kuhifadhia maiti na hospitali mbalimbali kugonga mwamba, na hatimaye wakaamini amepoteza maisha.

Nyaanga alianza maisha mapya baada ya kuondoka Kisii, na akafanikiwa kupata kazi, akaoa tena na kuanzisha familia mpya, huku maisha yake ya awali yakibaki kuwa siri.

Habari kuhusu Joseph zilifichuka hivi karibuni, baada ya mmoja wa majirani kumtambua na kumfahamisha chifu wa eneo hilo, na ndipo walipowafahamisha ndugu na jamaa zake ambao waliandamana nao kwenda kuthibitisha kama alikuwa ni ndugu yao. Famia yake ilipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa ni kweli aliliwa Nyaanga.

Baada ya mkusanyiko huo, familia ya Joseph imekataa kutoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo la kipekee na lenye msisimko mkubwa.

Send this to a friend