Mwanaume aomba mahakama ivunje ndoa yake kutokana na uzuri wa mkewe

0
43

Mwanamume mwenye umri wa miaka 40 kutoka nchini Zambia, Arnold Masuka, ameiomba mahakama kuvunja ndoa yake kutokana na urembo wa kipekee alionao mke wake.

Masuka aliwashangaza viongozi na mashahidi katika mahakama ya mji mkuu wa Lusaka wakati alipomwambia hakimu kwamba urembo wa mkewe, Hilda Mleya umemfanya kukosa usingizi mara kadhaa.

Mzaliwa huyo wa Lusaka ameongeza kuwa amekuwa akiishi kwa hofu kwa muda mrefu ya kumpoteza mke wake kwa mwanamume mwingine, na hata anahofia kumuacha mke wake nyumbani peke yake anapotaka kwenda kazini kwa kuogopa huenda akashawishiwa na wanaume wengine.

Asimamishwa kazi kwa kukausha bwawa la maji ili kutafuta simu yake

Mwanaume huyo amemtaja mke wake, Hilda anayetokea Gokwe nchini Zimbabwe, kuwa ndiye mwanamke mrembo zaidi aliyewahi kukutana naye.

Katika mazungumzo na wanahabari baada ya kesi hiyo, Karani wa mahakama hiyo, Chenjerai Chireya amekiri kwamba hajawahi kushuhudia tukio kama hilo mahakamani katika miaka yake yote ya utumishi.

Send this to a friend