Mwanaume apelekwa polisi kwa kwenda ukweni mikono mitupu

0
60

Kisa cha kustaajabisha kimetokea huko Bukwo nchini Uganda baada ya bwana harusi mmoja, Maikut Samuel (60) kukamatwa na familia ya mke wake kwa madai ya kwenda kwenye tukio la kujitambulisha bila kupeleka zawadi yoyote.

Inasemekana Maikut aliwataarifu wakwe zake kwamba atakwenda kwa ajili ya kumtolea mahari binti yao akiwa na ngo’mbe wanne na mbuzi watatu kama walivyokubaliana na aliahidi kwamba kila kitu kilikuwa tayari, lakini cha kushangaza alifika akiwa mikono mitupu na kuwaacha midomo wazi.

Watatu wakamatwa wakijaribu kubadilisha noti bandia benki

Baada ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya maandalizi hayo, wakwe hao waliamua kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi cha Bukwo, lakini baadaye familia zote mbili zililazimika kufikia makubaliano na kumlazimisha bwana harusi kusaini makubaliano ya kulipa shilingi milioni 1.9 ifikapo Desemba 30, 2023, ili aruhusiwe kumchukua bibi harusi.

Hili limezua hisia na mjadala miongoni mwa wananchi katika mitandao ya kijamii, huku wengine wakiunga mkono umuhimu wa kufuata tamaduni na wengine wakikosoa hatua hiyo kama isiyotenda haki.

Send this to a friend