Mwanaume apigwa kwa kuiba nguo za ndani za wanawake

0
38

Mwanaume mmoja amenusuruka kifo baada ya kushambuliwa na wakazi wa eneo la Kipkelion Mashariki, Kaunti ya Kericho nchini Kenya akidaiwa kuwa na tabia ya kuiba nguo za ndani za wanawake wa eneo hilo kwa makusudio yasiyojulikana.

Wakazi wa eneo hilo wamedai wanawake katika eneo hilo wamekuwa wakilalamikia kutoweka kwa nguo zao za ndani kutoka kwenye kamba zao za nguo pindi wanapozianika hali iliyosababisha kufanya mkutano wa dharura kujaribu kubaini anayefanya uhalifu huo.

Inaelezwa kuwa, wakati mkutano ukiendelea mwanamume huyo alikuwa kimya sana, na mara baada ya mkutano kumalizika mwanamume huyo na rafiki yake waliamua kwenda mtoni kuoga lakini walipokuwa wakielekea huko mshukiwa alitoweka kwa njia ya ajabu.

Inadaiwa aliingia kwenye nyumba na kuiba nguo za ndani za wanawake wa nyumbani hapo kabla ya kuungana tena rafiki yake mtoni. Lakini rafiki yake alipigwa na butwaa alipoona nguo ya ndani ikidondoka kutoka kwenye koti la mshukiwa, na kuvuta hisia za wanakijiji wengine waliokimbilia eneo la tukio.

Wanachi walipomkagua walimkuta na nguo za ndani kadhaa na walipofika nyumbani kwake kukagua walikuta nguo nyingi zaidi kutoka kwenye mifuko yake ndipo walipomshambulia kabla hajafanikiwa kutoroka.

Kulingana na jamaa wa mhalifu, mwanamume huyo aliwahi kunaswa akifanya matukio kama hayo huko Kuresoi, kaunti ya Nakuru kabla ya kufukuzwa kutoka eneo hilo.

Send this to a friend