Mwanaume mmoja jijini Nairobi nchini Kenya amepandishwa kizimbani kwa madai ya kuiba viatu na kompyuta mpakato ya mpenzi wake yenye thamani ya Ksh.25,000 (TZS 474,197) kisha kumpa mpenzi wake mwingine.
Mwanafunzi UDOM ajirusha ghorofani akidai amefelishwa makusudi
Ryan Lusalishi alifikishwa mbele ya Mahakama ya Sheria ya Makadara siku ya Alhamisi, ambapo mahakama imedai mshtakiwa aliiba kompyuta mpakato, begi na jozi ya viatu vya Elizabeth Okumu kati ya Novemba 7 na 8 mwaka huu jijini Nairobi.
Kulingana na Bi. Okumu ambaye alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkuu, Gathogo Sogomo amedai aliporejea nyumbani kwake alikuta baadhi ya vitu vimepangwa upya, na wakati alipokagua ndipo aligundua kuwa kompyuta ndogo, jozi ya viatu, begi na kadi ya ATM hazikuwepo.
Okumu ameiambia mahakama kuwa siku hiyohiyo, alipokea ujumbe wa muamala uliofeli wa PIN isiyo sahihi uliompa mashaka kuwa kuna mtu alikuwa akijaribu kutumia kadi yake ya ATM ambayo imeibwa na baada ya kujithibithishia kuwa hakuna mtu mwingine aliyeingia nyumbani alishuku kuwa ni mpenzi wake na kupiga simu polisi.
Amzika mtoto wa wiki mbili akiwa hai ili apate muda wa kujiuza
Mpenzi mwingine wa Lusalishi ambaye pia ni shahidi katika kesi hiyo aliyekamatwa na baadhi ya vitu hivyo nyumbani kwake, aliwaambia polisi wakati wa uchunguzi kuwa mwanaume huyo alirudi nyumbani na vitu hivyo na kumpa viatu ambavyo havikuwa saizi yake.
Mshtakiwa ameachiliwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena Januari 31 mwakani kabla ya kusikilizwa Mei 22.