Mwanaume, fanya mambo haya 10 uonekane ‘gentleman’ kwenye uhusiano

0
86

Mwanaume muungwana (gentleman) ni mtu ambaye ana mwenendo mzuri na wa heshima. Pia, muungwana ana sifa fulani zinazowatofautisha na wanaume wengine.

Kuwa muungwana kwa mwanamke kutamfanya ajihisi maalumu na pia utaonekana wa tofauti na wanaume walio wengi. Fuatilia namna bora  ya kuonesha uungwana wako kwa mchumba au mwenza wako;

1.Timiza ahadi zako
Moja ya sheria moja wapo ya kuwa muungwana katika uhusiano ni kuishi kulingana na maneno yako kila wakati. Unahitaji kufanya kila unachoahidi bila visingizio vyovyote.

2. Zungumza naye kwa heshima
Wakati wowote unapozungumza na mwenza wako, hakikisha unazungumza kwa heshima. Njia mojawapo ya kuwa muungwana katika mahusiano ni kuwa makini na maneno yako.

3. Iheshimu familia na marafiki zake
Kumbuka kwamba kuna watu wengine katika maisha yake ambao unapaswa kuwazingatia maana kabla ya kuwa naye, alikuwa na familia na marafiki ambao aliwajali.

4. Uwe tayari kuchukua hatua
Sifa mojawapo ya muungwana ni kuchukua hatua ya kufanya jambo fulani hata kama mambo yanapokuwa magumu. Usiwe tegemezi.

5. Kuwa na adabu unapokuwa hadharani
Ikiwa mtu yeyote atakukosea bila kujua, jaribu kujibu kwa adabu hata ikiwa una hasira.

6. Jifunze kuomba msamaha
Muungwana daima huomba msamaha kwa kosa lolote. Ukimkosea mpenzi wako, jifunze kuomba msamaha badala ya kuelekeza lawama au kujaribu kukataa kutokufanya.

7. Usisahau tarehe muhimu
Kukumbuka tarehe ni muhimu katika uhusiano.  Ikiwa unataka kujifunza jinsi ya kuwa muungwana katika uhusiano, hakikisha unakumbuka tarehe ambazo ni muhimu kwa mpenzi wako.

Mambo 4 yatakayokusaidia kuwa na utendaji kazi bora

8.Mfanye ajihisi mwenye furaha
Tunaishi katika ulimwengu uliojaa mafadhaiko ambapo tunatafuta njia za kurahisisha maisha yetu na kustarehesha zaidi. Jitahidi  kumfanyia mambo yanayoweza kumpunguzia msongo wa mawazo.

9.Mpe umakini wako, usimpuuze
Ikiwa una shughuli nyingi, hakikisha haumnyimi mwenzi wako umakini anaostahili.

Anataka pia kuwa na uhakika kwamba unamsikiliza. Kwa hiyo kuwa mpenzi ambaye unasikiliza.

10. Mpe uhuru wake
Ingawa uko kwenye uhusiano, kumbuka kuwa mwenzi wako anahitaji kufanya vitu anavyovipenda pia. Hatakiwi kuishi maisha kwa masharti yako.

Usilazimishe uchaguzi wako kwa mwenzi wako, badala yake unaweza kupendekeza na kuwaruhusu kufanya maamuzi yao.

Send this to a friend