Mwanaume wa miaka 40 adai ni mtoto wa Vera Sidika

0
42

Mwanamume mmoja (40) kutoka kaunti ya Busia nchini Kenya amejitokeza hadharani na kudai kuwa yeye ni mtoto wa mwanamitindo maarufu na mfanyabiashara nchini humo, Vera Sidika.

Mwanaume huyo anayejitambulisha kwa jina la Handsome Boy, amekuwa akieleza kuwa Vera alimtelekeza katika kijiji kimoja huko Kakamega alipokuwa bado mdogo, huku akisisitiza kuwa angependa kualikwa kwenye sherehe ya kuota meno ya binti yake Vera, Asia Brown.

“Mimi ni mtoto wa Vera Sidika na siogopi kusema, Vera mimi ni mwanao. Nimesikia mama yangu anamfanyia dada yangu sherehe ya meno ya kwanza angalau afanye hivyo au hata kuniruhusu niwe karibu na  dada yangu,” ameeleza.

Mwanamume huyo mwenye utata aliwahi kujitokeza hadharani mwezi Februari na madai yale yale ambayo Vera alikanusha akisema kuwa Asia ni mtoto wake wa pekee.

“Nitawezaje kupata mtoto mwingine na ninyi nyote bila kujua? Ninapenda watoto, angekuwa kwenye ratiba yangu yote kama Asia. Am even craving for a son right now,” Vera alijibu mashabiki wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram.

Hata hivyo Vera ameendelea kumkana kwa madai kwamba mwanaume huyo  ni mkubwa kuliko yeye, na kwamba hamfahamu.

Send this to a friend