Mwandaaji wa Miss Rwanda jela miaka mitano kwa ubakaji

0
47

Mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Rwanda, Dieudonne Ishimwe (36) maarufu Prince Kid amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la ubakaji na ushawishi wa kingono.

Prince Kid ambaye amewahi kuwa mwanamuziki alikamatwa Aprili mwaka jana akituhumiwa kuwadhalilisha kingono waliokuwa washiriki wa shindano hilo kisha akaachiliwa Desemba 2022 baada ya kuonekana hana hatia .

Hata hivyo, upande wa mashitaka ulikata rufaa na mahakama ya Kigali ikamkuta na hatia siku ya Ijumaa na kuamriwa pia kulipa faini ya faranga milioni mbili za Rwanda (Sawa na TZS milioni 4).

Wakili feki aliyeshinda kesi zote akamatwa

Kesi hiyo ilipelekea kusitishwa kwa shindano hilo la kila mwaka. Waendesha mashtaka walitaka ahukumiwe kifungo cha miaka 16 jela, lakini jopo la majaji watatu lilisema limetoa kifungo cha miaka mitano kulingana na ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Ishimwe kusihtakiwa kwa uhalifu.

Send this to a friend