Mwandishi wa habari afariki akiripoti mechi ya Argentina na Uholanzi

0
62

Mwanahabari mashuhuri wa Marekani, Grant Wahl amefariki dunia nchini Qatar baada ya kuzimia alipokuwa akiandika habari za Kombe la Dunia, Desemba 9, 2022 jambo lililozua mshtuko na huzuni katika ulimwengu wa michezo.

Kwa mujibu wa mashihidi waliokuwepo katika eneo la tukio wameeleza kuwa Wahl alianguka katika eneo la waandishi wa habari wakati akifanya kazi yake katika mchezo kati ya Argentina na Uholanzi huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijathibitishwa.

“Familia nzima ya Soka ya Marekani imevunjika moyo kujua kwamba tumempoteza Grant Wahl.

Grant alifanya soka kuwa kazi yake ya maisha, na tunasikitika kwamba yeye na uandishi wake mzuri hawatakuwa nasi tena,” Shirikisho la Soka Marekani limeandika kwenye wake wa Twitter.

Mayele na Mgunda wang’ara tuzo za Novemba

Mtangazaji mwenza, Chris Wittyngham amesema siku chache kabla ya kifo chake alikuwa akilalamika kujisikia vibaya ikiwemo kubanwa na kifua, hivyo alitafuta usaidizi katika kliniki ya matibabu katika kituo cha vyombo vya habari vya Kombe la Dunia.

Wahl amekuwa akiandika habari za soka kwa zaidi ya miongo miwili, na ameandika vitabu kadhaa vya michezo kulingana na tovuti yake.

Send this to a friend