Mwandishi wa Tanzania Daima afungiwa kwa kusambaza taarifa za mgonjwa wa corona

0
37

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Talib Hamad amesimamishwa kufanya shughuli za ukusanyaji, usambazaji au shughuli yoyote ya uandishi wa habari kwa muda wa mezi sita kuanzia leo Aprili, 2020.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar, Dkt. Juma Salum amesema mwandishi huyo amesambaza taarifa za mgonjwa wa virusi vya corona bila ridhaa ya mhusika.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria kitendo hicho si sahihi, hivyo Hamad amepewa adhabu hiyo kwa kukiuka maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Send this to a friend