Mwanga waanza kuonekana kuelekea tiba ya corona

0
32

Mmalaka ya Dawa na Chakula (FDA) nchini Marekani imeidhinisha matumizi ya dharura ya dawa ya Ebola, remdesivir, ianze kutumika kutibu virusi vya corona.

Kufuatia hatua hiyo, dawa hiyo itaanza kutumiwa na watu walioadhiriwa zaidi na homa ya mapafu (COVID-19).

Majaribio ya hivi karibuni yameonesha kuwa dawa ya remdesivir inayozalishwa na kampuni ya dawa ya Gilead ilisaidia kupunguza muda wa mgonjwa kupata ahueni ya COVID-19.

Hata hivyo wataalamu wametahadharisha kuwa dawa hivyo isichukuliwe kama ndio suluhisho la virusi vya corona, na kwamba FDA imeidhinisha matumizi ya dharura pekee.

Taasisi ya kupambana na magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani katika utafiti wake wa hivi karibuni ilibaini kuwa remdesivir inaweza kupunguza muda wa dalili kuonekana kwa muathirika kutoka siku 15 hadi siku 11.

Licha ya mafanikio hayo ya awali, bado ni kitendawili kama dawa hiyo inaweza kuzuia vifo vitaokanavyo na virusi vya corona.

Send this to a friend