Mwanza: Watu sita wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

0
41

Watu sita wamefariki papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hilux namba T476 DZL wakati wakifanya mazoezi (jogging) eneo la Shule ya Msingi Lumala wilayani Ilemela mkoani Mwanza majira ya saa 12 asubuhi.

Akizungumza na Swahili Times, Kaimu Makanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa wakati wakifanya mazoezi ambayo wamekuwa wakiyafanya kila Jumamosi, lilitokea gari hilo na kuwagonga kwa nyuma kisha dereva kutoroka kusikojulikana.

Kaimu Kamanda amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo pamoja na kumsaka dereva wa gari hilo ambaye ametoroka.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu ashikiliwa kwa kudaiwa kumuua mwalimu

Ameeleza kuwa kati ya majeruhi hao 14, majeruhi wanne wanapatiwa matibabu katika Hosipitali ya Bugando na wengine 10 wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Sekou-Toure mkoani humo.

Aidha, amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Shedrack Safari, Selestine Safari, Makorongo Manyanda, Peter Fredrick, Hamis Wariri na Aman.

Send this to a friend