Mwanzilishi wa Tiktok sasa ndiye mtu tajiri zaidi nchini China

0
47

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya ByteDance, ambayo inamiliki TikTok, Zhang Yiming ndiye tajiri mpya nchini China kwa mujibu wa Ripoti ya 2024 ya Hurun China Rich List.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utajiri wa Zhang umefikia dola bilioni 49.3 [TZS trilioni 134.3], hasa kutokana na ongezeko la mapato ya ByteDance kwa asilimia 30 mwaka uliopita, yakifikia dola bilioni 110 [TZS trilioni 299.7].

Tangu kuzinduliwa rasmi kwa TikTok mwezi Mei 2017, imepata umaarufu mkubwa duniani na kuvutia watumiaji wengi, hasa vijana. TikTok imekuwa pia mfano wa mafanikio kwa kampuni za Kichina zinazotaka kuvuka soko la Marekani na kimataifa.

Mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 41 aliacha nafasi yake ya uongozi kama Mkurugenzi Mtendaji na mwenyekiti wa ByteDance mwaka 2021, lakini inaaminika kuwa anamiliki takriban asilimia 20 ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, TikTok inakabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na kesi zinazohusiana na usalama wa watoto na inapanga kuipiga marufuku mwaka 2025 isipokuwa kama ByteDance itaiuza.

Idadi ya mabilionea nchini China imepungua kwa kiasi kikubwa, huku jumla ya utajiri ukiripotiwa kushuka hadi dola trilioni 3, ikiwa ni upungufu wa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Send this to a friend