Mwendokasi Mbagala kuanza Machi 2023

0
99

Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema usafiri wa mabasi yaendayo haraka kwa barabara ya Mbagala kuelekea Gerezani utaanza Machi 2023.

Ameyasema hayo Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Edwin Mhede wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) ilipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt. Mhede amesema  malengo ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha wanakwenda kutoa huduma bora ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam ambayo itachochea uchumi kukua.

LATRA: Kondakta lazima awe na cheti na asajiliwe

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Abdallah Chaurembo ambaye pia ni Mbunge wa Mbagala amesema mradi huo uko vizuri na kushauri waendelee kuboresha baadhi ya kasoro.

Send this to a friend