Mwenye nyumba afumaniwa na mke wa mpangaji wake

0
48

Mwenye nyumba, Mathayo Gote, Mkazi wa Kijiji cha Kibwela mkoani Geita ameadhibiwa kwa kuchapwa fimbo hadharani na kutozwa faini ya TZS 200,000 baada ya kufumaniwa na mke wa mpangaji wake.

Akisimulia tukio hilo, mpangaji huyo, Emmanuel Ndarahu amesema baada ya kuhamia nyumbani kwa mzee Gote aliona mazoea ya mara kwa mara na mkewe mdogo ikiwemo kumpa pesa.

Ameeleza baada ya kuona mazoea kuzidi alimfuata mwenye nyumba wake na kumuonya kuhusu uhusiano wake na mkewe huku akimpiga mkewe kwa kitendo hicho.

“Ilibidi nimuonye mzee kwamba nilimpiga mke wangu, sikukusudia ila nimempiga kwa sababu ya hili tukio uliliofanya mwenyewe, ebu naomba hii tabia uache, maana mimi natoka ndani nakuita baba, wanangu wanakuita babu, unakuja hapa unapikiwa chakula kama kawaida. Likawa limeisha,” amesimulia.

Nchi 10 za Afrika ambazo watu wake wana furaha zaidi

Ameendelea kusimulia kwamba siku kadhaa baada ya kumuonya alimshuhudia mwenye nyumba akiingia chumba cha mke wake mdogo mara (Ndarahu) alipotoka kwenda msalani dakika chache baada ya wao kuingia kulala na ndipo alipoingia ndani na kumkuta akiwa na nguo ya ndani pekee.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Simeon Kisinza amesema hiyo ni mara ya tatu anakamtwa na mke wa mtu hivyo baada ya tukio hilo, ofisi ya kijiji iliamua kumpeleka kwa Wananzengo na kupatiwa adhabu ikiwemo kuchapwa viboko pamoja na kulipa faini.

Send this to a friend