Kiongozi wa CHADEMA ashikiliwa kwa kuhamasisha uvamizi kwa wasimamizi wa uchaguzi

0
31

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mkoa wa Kilimanjaro, Gervas Eliewaha Mgonja, (42) kwa kosa la kutoa kauli za kuhamasisha wananchi kuvamia makazi ya wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya kuonekana kwa video mjongeo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akiwa anawahamasisha wananchi kufanya vurugu Novemba 27, 2024.

SACP Maigwa ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo anachukuliwa maelezo ili hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa yeyote atakayethubutu kufanya vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjifu wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Send this to a friend