Mwenyekiti na Balozi wake wahukumiwa jela maisha kwa jaribio la kuua

0
136

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imewahukumu kifungo cha maisha jela watu watano, wakiwemo mwenyekiti wa kijiji na balozi wake, baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuua kwa kumwagia tindikali mkazi wa kijiji cha Nyamasere, Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza.

Watuhumiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo mnamo Septemba 1, 2022, ambapo walimvamia na kumwagia tindikali William Buyeye, ambaye ni mkulima na mkopeshaji wa fedha katika kijiji hicho.

Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Jaji Athuman Matuma amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, ambao uliwaunganisha moja kwa moja watuhumiwa hao na tukio hilo.

Hata hivyo, Mahakama imewaachia huru watuhumiwa wengine wanne baada ya ushahidi dhidi yao kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo.

Aidha, Wakili wa utetezi Sekundi Bartholomeo amesema hawajaridhishwa na uamuzi wa Mahakama na wamepanga kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Send this to a friend