Mwenyekiti wa ADC awaonya wanachama wasiomheshimu Rais Samia

0
51

Chama cha Alliance for Democratic Change kupitia Mwenyekiti wa chama hicho, Hamad Rashid Mohamed kimewaonya wanachama wa chama hicho wasiomheshimu Rais Samia Suluhu Hassan.

Ameyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha ADC jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa Rais Samia anapaswa kuungwa mkono na si kumkebehi.

“Rais amefungua milango ya demokrasia nchini anapaswa kuungwa mkono na siyo kebehi na dhihaka, nani asiyejua kuwa vyama vya upinzani nchini vilikuwa kifungoni? Nikiwa kama Makamu Mwenyekiti wa Kikosi kazi sipo tayari, na ADC haipo tayari kuona Rais anakashifiwa kwa namna yoyote, na kama kuna anayefikiria kufanya hivyo ndani ya ADC basi si mahala pake,” amesema Hamad.

Aidha, ameongeza kuwa wanachama wa ADC wasiache kukikosoa kistaarabu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapokosea na kwamba kwa kufanya hivyo ndio uungwana.

Send this to a friend