Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ashambuliwa Dodoma

0
47

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo jijini Dodoma.

Taarifa ya Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA inaeleza kuwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani na amekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Aidha, Makene amesema tukio zima lina muonekano wa kisiasa kutokana na hivi karibuni baadhi ya watu kutoa maneno ya uchonganishi dhidi yake.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto amesema amepata taarifa za Mbowe kushambuliwa na watu watatu na kuvunjwa mguu wa kulia, hivyo wanafuatilia na jeshi la polisi litatoa taarifa kamili.

Chama kimesema kwa muda muafaka kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo.

Send this to a friend