Mwigizaji Idris Elba kufungua studio ya filamu nchini

0
43

Mwigizaji maarufu wa filamu duniani kutoka Uingereza ambaye ni Balozi Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (IFAD), Idris Elba ameonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania kwa kufungua studio kubwa ya filamu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus wakati akitoa taarifa muhimu kuhusu ziara za Rais Samia Suluhu Hassan amesema mazungumzo yaliyofanywa na Rais Samia na mwigizaji nchini Uswisi yamezaa matunda kwa kuwa si Tanzania pekee itakayonufaika endapo mazungumzo hayo yatafanikiwa .

“Mazungumzo ndo kwanza yanaanza lakini hayo yakifanikiwa ina maana hiyo studio itaweza kusaidia si Tanzania lakini Afrika Mashariki na kati,” ameeleza Zuhura.

Aidha, amesema katika ziara yake nchini Uswisi Rais Samia amefanya mikutano na wawekezaji mbalimbali wakubwa duniani kuhusu fursa mbalimbali zilizopo nchini Tanzania kupitia sekta za kilimo, utalii, kilimo na kadhalika.

Mashabiki wa Arsenal wakamatwa wakisheherekea kuifunga Manchester United

Katika mkutano wake nchini Senegal uliohudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali 34 za bara la Afrika amesema moja ya mambo yaliyozungumziwa ni ongezeko la hali ya vyakula duniani ulioathiwa na vita vya Ukraine na UVIKO-19 ambapo pia wameazimia kila nchi kukamilisha mipango wa uwekezaji katika kilimo pamoja na kuongeza bajeti ya taifa katika kuendeleza kilimo.

Send this to a friend