Mwigulu aishauri serikali isitangaze visa vipya wa corona

0
53

Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba ameishauri serikali kutotangaza visa vipya vya maambukizi ya virusi vya corona, kwa kile alichobainisha kuwa baadhi ya watu wanatamani kuona idadi ya wagonjwa wa COVID-19 nchini inaongezeka.

Akizungumza katika kikao cha bunge la bajeti mjini Dodoma amependekeza kuwa taarifa zitolewa za aina tatu tu ambazo ni kuwaeleza wananchi kwamba ugonjwa upo ili wandelee kuchukua tahadhari, taarifa za wagonjwa waliopona na wale waliofariki.

“Na mimi nilivyokuwa nawaza, naona hata taarifa tunazozitoa zibaki za aina tatu. Tutoe taarifa ya kwamba hili gonjwa bado lipo, tutoe taarifa ya waliopona na tutoe taarifa labda ya wale ambao imekuwa bahati mbaya sana,” amesema mbunge huyo.

Amesema utaratibu uliopo sasa wa nchi kutaja idadi ya wagonjwa haujakaa sawa kwani nchi zinakuwa kama zinashindana.

Aidha, amewataka viongozi kutogeuza jambo hilo kuwa mtaji wa kisiasa badala yake wawe na kauli moja, na kama ni siasa ifanyike kwenye mambo yaliyopo kwenye ilani.

“Niwapongeze sana viongozi wa kidini wametuzidi wanasiasa, wanaongelea jambo hili [corona] kwa umakini mkubwa,” amesema Mwigulu.

Ameongeza kuwa kauli za viongozi zinapswa kuwahimiza wananchi kila mmoja kwa nafsi yake kubadili tabia ili kukabiliana na janga hili.

Send this to a friend