Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

0
28

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.


Uteuzi wa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba unaanza leo tarehe 02 Mei, 2020.


Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia jana tarehe 01 Mei, 2020.

Send this to a friend