Mwili wa Mtanzania aliyekuwa anafanya kazi Google waopolewa Mto Miami, Marekani

0
54

Mwili wa Mtanzania, Abraham Mgowano (35) aliyekuwa akiishi nchini Marekani umekutwa ukielea kwenye Mto Miami, Jimbo la Florida nchini humo baada ya kuripotiwa kuanguka kutoka kwenye boti Februari 24 mwaka huu.

Polisi wamesema walipokea simu ya mtu kutoka eneo la tukio akisema ameona mwili ukiwa unaelea mtoni siku ya Jumanne Februari 27 ikiwa ni siku tatu toka Abraham aripotiwe kuanguka kutoka kwenye boti siku ya Jumamosi Februari 24, 2024 saa mbili usiku.

Aidha, kituo cha televisheni cha 7news cha nchini Marekani kimeripoti kuwa
Abraham alipata ajali hiyo akiwa na wenzake 12 ambapo polisi walianza kumtafuta bila mafanikio hadi walipopata taarifa za kupatikana kwa mwili huo.

Abraham alikuwa kati ya wanafunzi bora 12 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2007 akitokea Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam, ambapo yeye na wenzake walipata nafasi ya kukutana na kupongezwa na Rais wa Tanzania wakati huo, Dkt. Jakaya Kikwete.

Nchini Marekani, Abraham alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Google kwa miaka tisa baada ya kuwa mmoja wa wanafunzi bora kutoka Chuo Kikuu cha Stanford.

Send this to a friend