Mwili wa Rais Mugabe watakiwa kufukuliwa

0
37

Grace Mugabe, Mke wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametakiwa kufika mbele ya mahakama ya kitamaduni kufuatia madai ya kukiuka kanuni za mazishi ya mwili wa mumewe.

Mjane huyo anadaiwa kukiuka tamaduni kwa kumzika mumewe nyumbani (homestead) badala ya eneo lililochaguliwa na ndugu na mama wa marehemu.

Barua kutoka kwa Chifu Zvimba, chifu wa eneo alikozaliwa Rais Mugabe, kwenda kwa Grace imemuelekeza mjane huyo kufukua mwili huo ili uzikwe upya kwa mijibu wa taratibu za watu wa Zvimba.

Aidha, ametakiwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka tamaduni.

Mugabe alifariki duni mwaka 2019 nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95. Alizikwa katika eneo la Katuma, wilayani Zvimba, baada ya mvutano kati ya serikali na familia kuhusu eneo la kumzika.

Mmoja wa wanafamilia amenukuliwa akisema kuwa mazishi ya Mugabe yalizingatia matakwa yake, na kuwa hakuna mgogoro ndani ya familia hivyo jambo hilo lipo juu ya mamlaka ya Chifu.

Send this to a friend