Mzaliwa wa Rwanda akamatwa Uganda kwa madai ya ujasusi

0
44

Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Uganda vinamshikilia Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu (kibinafsi) cha Victoria, Dkt. Lawrence Muganga kwa madai ya ujasusi na kuishi nchini humo kinyume cha sheria, amesema msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali, Flavia Byekwaso.

Dkt. Muganga ambaye ni mzaliwa wa Rwanda alichukuliwa na maafisa ambao hawakuwa wamevaa sare kutoka katika ofisi yake mjini Kampala Alhamisi mchana.

Byekwaso amesema uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi ya mwanazuioni huyo zinaendelea.

Hata hivyo, haijulikani iwapo kukamatwa kwake kuna uhusiano na mvutano kati ya Rwanda na Uganda. Kuna nyakati uhusiano baina ya nchi hizo mbili hutetereka, huku kila upande ukimlaumu mwenzie kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi ya mwenzake.

Send this to a friend