Mzee ‘aliyepigwa’ risasi na Polisi kukatwa mguu, IGP aagiza uchunguzi

0
62

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillius Wambura amemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufuatilia tukio la mzee Abdallah Mohammed Ngombo mwenye umri wa miaka 75, mkazi wa Mkuranga aliyedaiwa kupigwa risasi mguuni na Askari Polisi nyumbani kwake wakati wakiwa katika operesheni.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime amesema Jeshi la Polisi Makao makuu limesikia taarifa hiyo na kilio cha wanandugu, hivyo linafanya uchunguzi ili haki iweze kutendeka.

“Jeshi la Polisi Makao makuu limesikia maelezo na kilio cha wanandugu pamoja na taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji. Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Camillius Wambura amemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kufuatilia tukio hilo na kufanya uchunguzi kwa kina ili haki iweze kutendeka kama wanandugu walivyoomba,” amesema.

Mwanafunzi atolewa korodani baada ya kupigwa na walimu wake

Inadaiwa katika tukio hilo, Polisi walifika nyumbani kwa mzee huyo wakiwa na mtuhumiwa ambaye aliwapeleka nyumbani hapo kwa shutuma za wizi, na ndipo lilipotokea tukio hilo la kupigwa risasi.

Naye kijana wa mzee huyo, Mohammed Ngombo amesema kwa sasa mzee Abdallah amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu, na kwamba madaktari wameshauri akatwe mguu wake ili kuepusha madhara mengine zaidi.

Send this to a friend