Mzee atangaza kuwaozesha wake zake kwa mwanaume anayewataka

0
60

Mzee mmoja anayejulikana kwa jina la Lusanika Malunguja mkazi wa Kijiji Cha Nyamgogwa wilaya ya Nyan’ghwale mkoani Geita amewashangaza watu wengi kufuatia kitendo cha kuwaozesha wake zake pindi wanaume wanapowahitaji.

Malunguja ambaye anajishughulisha na kilimo amesema sababu za kufanya hivyo ni kutokana na kila akioa mwanamke  mzuri wanaume wanampenda kutokana na yeye kuwa masikini, hali inayosababishwa na yeye kuishi na familia kubwa nyumbani kwake.

Ameongeza kuwa mpaka sasa amekwishaozesha wake zake wawili, na kwamba hata sasa mwanaume yeyote anayetaka kumuoa mke wake anamruhusu, kikubwa anachokitaka ni mwanaume huyo kuelewana na mke wake kwanza kisha afike nyumbani kutoa mahari.

“Hayo masuala yalinitokea kwa sababu nilikuwa masikini sana nilikuwa sina chochote watu wananicheka nikileta mwanamke mzuri wanampenda kwa sababu nipo masikini, umasikini ulikuja kwa sababu ya kuishi na watu mia moja, watu wakawa wanawapenda wake zangu,” amesema Malunguja.

Sababu 5 zinazosababisha tatizo la ganzi mwilini

Ameongeza, “watoto nawashukuru sana kwa sababu walichukua mke wangu wakaja kujisalimisha na ukali ukatoka, na mimi sio mkali walipokuja wakanipa ng’ombe tatu.  Mara ya pili mwingine wakaja tena wakatoa mahari kwa mke wa pili, hata sasa akija mwingine asiniulize mimi aende kwa mke wangu akamuulize, mwanamke akikubali mahali watapanga wenyewe wataniletea.”

Send this to a friend