Mzee atuhumiwa kuchoma moto nyumba ya mpenzi wake kisa wivu

0
59

Nestory John (52) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya mpenzi wake, Eva Stephano na kusababisha vifo vya watu watatu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa tukio hilo lilitekelezwa Desemba 07 mwaka huu katika mtaa wa Lwanhima jijini humo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Wazazi jela maisha kwa kumuua binti yao aliyekataa kuolewa na binamu yake

Kamanda Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza tukio hilo, alikimbilia kwa mganga wa kienyeji kuanguliwa ili asiweze kukamatwa na polisi.

Aidha, mtuhumiwa amebainika kuwa na jeraha usoni ambalo limetokana na moto, jambo ambalo linaashiria mtuhumiwa alipata jeraha hilo pindi moto ulipolipuka wakati akitekeleza tukio hilo.

Send this to a friend