Mzee Mutasa aliyehitimu PhD akiwa na miaka 82, afariki dunia

1
60

Dkt. Samwel Mutasa, msomi aliyetimiza kiu yake ya kuhitimu Shahada ya Uzamivu mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 82, amefariki nchini Marekani.

Binti yake mkubwa Linda Mutasa ambaye alikuwa akiishi naye jijini Dar es Salaam wakati wa masomo yake amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake na kusema kuwa hivi karibuni alisafiri kwenda Marekani kwa ajili ya kuwaona watoto wake ambao wanafanya kazi huko.

Anaeleza kuwa, baada ya muda baba yake alikuwa akilalamika kupata maumivu ya kichwa, walipotoa nyumbani na waliporudi walimkuta amelala chini na hawezi kuzungumza badala yake alionyesha ishara kuwa anasikia maumivu makali ya kichwa.

Dkt. Mutasa alikimbizwa hospitalini na madaktari waligundua kuwa, mshipa wa damu umepasuka katika ubungo wake na baada ya siku tatu alipoteza maisha.

Jina la Dkt. Mutasa lilifahamika zaidi baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu katika uchanganuzi wa kemikali wa virutubishi vya mimea na dawa (chemiacal analysis of certain nutrients and medicinal plants of the Genus Cassia) ambapo safari yake ilianza miaka 41 kabla ya kuhitimu kwake na pia alidai kuwa lengo lake si kupata kazi wala pesa bali kuongeza upeo na maarifa.

Send this to a friend