Mzee Shamte amwomba msamaha Rais Dkt. Mwinyi

0
60

Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi, Baraka Shamte amemwomba radhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi kufuatia kauli yake aliyoitoa mtandaoni.

“Kwa heshima na taadhima, ikizingatiwa kuwa mimi sijawahi kufanya kosa katika umri wangu huu, nimeomba nisamehewe, nirudishiwe kadi yangu ya Chama cha Mapinduzi,” amesema.

Shamte ameahidi kuwa mwaminifu, mkweli na mthabiti na kuahidi kutorudia kosa alilolifanya na kuongeza kuwa yeye ni kada wa Chama cha Mapinduzi.

Hivi karibuni, Shamte alionekana kwenye mitandao ya kijamii akihojiwa na kusema haridhishwi na utendaji kazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), hivyo Rais Mwinyi akimaliza miaka mitano, awapishe wengine wagombee.

Baada ya maneno hayo Chama cha Mapinduzi Zanzibar kilitangaza kumvua uanachama kwa madai kuwa hakumheshimu Dkt. Hussein Mwinyi.

Send this to a friend