Mzee wa miaka 65 ajinyonga kisa wivu wa mapenzi

0
59

Mwanaume wa miaka 65 aliyejulikana kwa jina la Bakari Mtepa mkazi wa Kijiji cha Majengo Halmashauri ya wilaya ya Mtwara amefariki baada ya kujinyonga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, Mtaki Kurwijila amesema tukio hilo limetokea Februari 18, mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi baada ya kutoweka nyumbani kwake Februari 12 na kwenda kusikojulikana baada ya kutoelewana na mke wake.

“Mwili wa Mtepa ulikutwa umefungwa na mtandio shingoni ukiwa umening’inia kwenye tawi la mkorosho na sababu za kujinyonga, inasadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi baada ya kumtuhumu mke wake kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine,” amesema Kamanda.

Aidha, ameeleza kuwa “kwa mujibu wa taarifa tulizozipata katika eneo la tukio, kuna karatasi iliyokuwa imeandikwa ikielezea sababu hizo alizochukua kujinyonga na mwili wale umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Lingula kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.”

Send this to a friend