Nabi: Morrison hana pumzi ya kutosha uwanjani

0
29

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema mchezaji na winga wa klabu hiyo, Bernard Morrison hapewi muda mwingi wa kucheza uwanjani kwa sababu hana pumzi ya kutosha.

Nabi amebainisha kuwa hali hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kutopenda mazoezi makali na hivyo kushindwa kuhimili kucheza uwanjani kwa muda mrefu.

“Watu wengi wanataka kumwona Morrison anacheza lakini sisi makocha ndio tunajua ubora wa kila mchezaji kwa kila dakika kuanzia mazoezini mpaka uwanja wa mchezo,” amesema.

Ameongeza kuwa “Morrison wa sasa ni vigumu kumpa muda zaidi ya huu tunaompa labda abadalike kwa kujiweka tayari zaidi, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana ndio maana tulimleta hapa lakini kwasasa hayuko tayari kucheza kwa muda mrefu zaidi ya huu tunaompa watu waelewe hili.”

Rais wa FIFA aipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu

Aidha, akieleza kuhusu mchezo wa marudiano ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaofanyika Juni 03, 2023 nchini Algeria, amesema anaamini klabu ya Yanga inakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo kutokana na maandalizi ya kutosha waliyoyafanya.

Send this to a friend